Namba: +255 (0) 679 925 725 Barua pepe: info@sokokuuchifukingalu.co.tz

Soko la chifu kingalu, Morogoro Tanzania

Soko la chifu kingalu linapatikana halmashauri ya mji wa morogoro, Ni miongoni mwa soko bora sana na la kisasa hapa nchini. Soko hili linapatikana katikati ya mji wa morogoro kadiliwa 2 mpaka 3 kilomita, kutoka mzunguko unaogawanya barabara ya Dodoma, Dar es salaam na Iringa (Msamvu).

Soko letu

Ofisi

katika soko hili la kisasa la chifu kingalu kuna ofisi ambazo zinashughurika na utoaji huduma na uuzaji wa bidhaa mbalimbali.

Maghara yakuhifazia bidhaa & chakula

Soko hili la kisasa pia lina huduma ya uhifadhi nafaka na bidhaa mbalimbali za wafanyabiashara wa ndani na nje ya soko kupitia maghara yaliopo.

Taasisi

kulingana na utofauti na upekee wa soko la kingalu umepelekea baadhi ya mataasisi mbalimbali kuanzishwa ndani ya soko.

Maduka ya Kisasa

Maduka ya kisasa na yenye kutoa huduma za kidigitali yameanzishwa ndani ya soko hili yaliopelekea huduma kuwa rahisi na ya huhakika wakati wote.

SHUGHURI ZILIZOMO

Fulsa mbalimbali zimeongezeka kutokana na kuanzishwa kwa soko hili la kisasa, pia kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu ndani na nje ya mji wetu kupitia shughuri zinazofanyika eneo la soko kuu na maeneo yote ya karibu, makundi mbalimbali yamepata fulsa kulingana na huitaji wa huduma za kijamii.

  • Biashara Ndogondogo

    Karibu soko la chifu kingalu ujionee na ujipatie huduma na bidhaa zitolewazo na wafanya biashara wadogo wadogo na machinga katika maeneo yao maalumu ya kufanya biashara zao yaliyopangwa na yenye miundombinu mizuri kiusalama muda wote.

  • Huduma za Usafirishaji (Abiria na Mizigo )

    Miundombinu imara iliyojengwa kwa lengo la kutanua fursa ndani ya soko limeoneshwa vizuri katika idara ya usafirishaji wa mizigo na abiria ndani na nje kupitia boda boda, gari za kukodi na bajaji.

  • Huduma za Afya

    Mabadiliko ya miundo mbinu hususani katika mazingira ya soko kumepelekea uanzishwaji wa taasisi za utoaji huduma za afya ziendeleazo ndani ya soko zikilenga wanajamii wote wa ndani na nje ya soko huduma hizo zikitolewa na taasisi binafsi, pia uwepo wa maduka ya madawa baridi za binadamu na mifugo kunaleta chachu ya mzunguko mkubwa wa kibiashara.

  • Taasisi za fedha

    Huduma za kifedha zinazotolewa na taasisi za fedha, na ofisi mbalimbali za uwakala wa fedha pamoja na ofisi za mikopo, zinaleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi ndani ya soko letu.

  • Ofisi mbalimbali

    Uwepo wa ofisi zinazotoa huduma mbalimbali ndani ya soko letu kunapelekea mwingiliano mkubwa wa kijamii na ukuzaji wa uchumi katika eneo la soko.

Dhima


Matangazo ya Biashara

ToTovuti hii inatoa fulsa kwa wafanyabiashara wote kutangaza bidhaa na huduma zao, mteja anauwezo wa kuona fremu huduma na bidhaa zilizomo kwa pamoja & wamiriki wa fremu, Vizimba na Mteja anaweza kuoda, kununua bidhaa au kupata huduma anayoihitaji ndani ya soko mtandaoni kupitia matangazo ytakayokua yanarushwa.

Umoja wa wafanyabiashara

Uwepo wa vyama mbalimbali ndani ya soko hili umepelekea kuanzishwa kwa umoja wa wafanyabiashara, vikundi vidogo vidogo vyenye uongozi ndani yake & umoja huu unachangia mabadiliko makubwa ya kibiashara sokoni hivyo kupitia tovuti hii wafanyabiashara wanaweza kujuana na kuungana kupitia aina ya bidhaa zao zikiwa na uwiano kwani tovuti hii itaonesha bidhaa zote na huduma zipatikanazo sokoni pamoja na mhusika wa huduma.

Makundi ya kijamii mtandaoni

Wafamyabiashara wote wa ndani ya soko wataungwa katika makundi ya mitandao ya kijamii kwa ujumla wao ikiwa makundi hayo yatausisha na wanajamii tofauti tofauti & lengo au kusudio ni kuongeza mwingiliano baina ya wafanyabishara na jamii inayozunguka.

vikundi Vidogo vodogo

Uwepo wa vikundi hivi uchangia chachu ya upatikanaji na uwezeshwaji wa mikopo yenye riba nafuu kwaajili ya maendeleo yao & Manufaa yaliopatikana yameonekana kupitia ukuzwaji wa pato la mmoja mmoja kwa wanachana wote.

Mambo ya Kibiashara

Uwepo wa midahalo/Mijadala mbalimbali inayohusu biashara na mafanikio, uendeshwa kwa lengo kuu la kukuza na kubadili uchumi wa kila mfanyabiashara kupitia mawazo yao mbali mbali wayatoayo juu ya mitazamo yao.

Shughuri za Kiutawala

Utuliwa wa soko unajengwa na shuguri bora za kiutawala zilizopo sokoni hapa, vikao baina ya wafanyabiashara na viongozi imnaleta jita kwa maendeleo ya soko.

Maduka yanayopatikana ndani ya soko kuu chifu kingalu

Tangaza Nasi Kupitia Tovuti, Instagram, Facebook na Twitter ndani na nje ya Morogoro

Wanakingalu kwa pamoja tunaweza