Namba: +255 (0) 679 925 725 Barua pepe: info@sokokuuchifukingalu.co.tz

Soko Mnadani

Tangaza huduma na bidhaa yako Sokoni kwetu
Kupitia tovuti na kurasa zetu za kijamii


HUDUMA ZIENDELEAZO NDANI YA SOKO LA chifu KINGALU

Maghara ya madawa

Huduma za dawa (binadamu na mifugo) zinapatikana ndani ya soko, Dawa za binadamu zinatolewa kwa jumla na rejareja na MedLife Pharmacy na Dawa za mifugo zinatolewa pia kwa jumla na rejareja na Royal Agrovet & Heri Agrovet hawa ni baadhi ya mawakala wa uuzaji na usambazaji dawa kwa bei nafuu ndani na nje ya morogoro.

Huduma za usafiriji

Usafirishaji wa ndani na nnje ya soko unafanyika kwa utaratibu usio mkera mteja, vyombo vya usafiri vilivyopo ni pamoja na bajaji, bodaboda pamoja na magari makubwa BM Coarch , safari zao za ndani ya wilaya na nje ya mkoa wa Morogoro.

Huduma za simu

Je unamfahamu wakala mkubwa na watengenezaji wa simu zilizoharibika morogoro, au umewahi kuwasikia Carl Care & BB ELECTRO-TECH , hawa ni baadhi ya mabingwa wa u hawa ni baadhi ya mabingwa wa utengenezaji simu zilizoharibika , wanapatikana ndani ya soko la chifu kingalu.

Huduma za tehama

Teknologia inazidi kushika hatamu ndani na nje ya nchi,katika soko la chifu kingalu huduma zote za tehama zinatolewa na SkyLink Solutions & Penta M , ambao wameamua kutia nanga ndani ya soko la chifu kingalu Morogoro, kwa lengo la kuimarisha misingi imara ya teknolojia na sanaa katika jamii

Huduma za mtandao

Huduma za kimtandao zimekufikia kupitia watoa huduma za mitandao We Konnect Morogoro, pia ni wakala wa mtandao wa satelaiti TANZANIA na nchi jirani, kwa huduma bora na safi za mtandao wa maofisini, mahotelini, majumbani wafikie hawa, hawakuishia hapo tena wanaonyesha utofauti mkubwa sana kwa kuwa huduma zao zinafanya kazi vizuri hadi vijijini

Migahawa ya Vyakula

Migahawa ya kisasa yenye mazingira bora na miundombinu safi iliyo ndani ya soko pamoja na vyakula bora kwa ujumla, vinapatikana kwa bei ya kizalendo(inayokidhi hali ya kiuchumi ya watanzania wote) wa ndani na nje ya soko.

******

JE UNA SWALI LOLOTE LA KULIZA ?

Kama unatamani kufahamu zaidi kuhusu swala lolote linalohusiana na hughuri zote za sokoni na kazi zetu, tufikie kwa kuuliza swali kwenye fomu hapo chini

Ujumbe wako umeufikia. Ahsante!

Maudhui kila wakati

Tangaza huduma na bidhaa zako nasi kila wakati, matangazo yatawafikia wateja ambao wapo nje na ndani ya eneo la biashara yako, na kuongeza namba ya wateja na kipato chako

Ofa

Kwa Wafanyabiashara wote wa ndani ya soko kutakuwa na ofa maalumu mara kwa mara,lengo ni kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara na kutanua wigo wa wateja.



Huduma kwa wateja (24/7)

Kwa msaada wa haraka au unaohusiana na maswala ya kifundi kwa huduma zote tufikie kwa njia ya;
(i) Ana kwa Ana (Tembelea ofisini)
(ii) Kwa njia ya mtandao (tovuti, simu, mitandao ya kijamii) . .

Wateja Endelevu (wa mara kwa mara)

Kwa washiriki wetu watakao unganishwa na mfumo wa matangazo na kuwa nasi mara kwa mara katika huduma zetu kutakua na punguzo, pendeleo katika vifurushi vyetu vya malipo kama vile ofa mbalimbali ikiwemo; "Twenzetu kileleni" ikiwa na maana ya nunua kifurushi tukupandishe cha juu yake.